Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Uvumbuzi wa Kiakiolojia Unaonyesha Mfalme Daudi Alikuwa Mtu Halisi

Uvumbuzi wa Kiakiolojia Unaonyesha Mfalme Daudi Alikuwa Mtu Halisi

 Kulingana na Biblia, Mfalme Daudi wa Israeli aliishi katika karne ya 11 K.W.K. na wazao wake walitawala kwa mamia ya miaka. Lakini wachambuzi fulani wamesema kwamba Daudi alikuwa mtu wa kuwaziwa ambaye alibuniwa miaka mingi baadaye. Je, Mfalme Daudi alikuwa mtu halisi?

 Mwaka wa 1993, mwanaakiolojia Avraham Biran na kikundi chake waligundua kipande cha jiwe huko Tel Dan, kaskazini ya Israeli, ambacho kilikuwa na maandishi yaliyorejelea “Nyumba ya Daudi.” Maneno hayo yaliyoandikwa kwa maandishi ya zamani ya Kiyahudi, yanakadiriwa kuwa yaliandikwa karne ya tisa K.W.K. Inaonekana kipande hicho kilikuwa sehemu ya mnara uliosimamishwa na Waaramu, wakijivunia ushindi mbalimbali dhidi ya Waisraeli.

 Makala katika jarida Bible History Daily inasema hivi: “Watu fulani hawakuamini maandishi ‘Nyumba ya Daudi’ . . . Hata hivyo, wasomi wengi wa Biblia na waakiolojia wanakubali bila kubisha kwamba jiwe la Tel Dan ni uthibitisho imara wa kwanza nje ya Biblia kwamba Mfalme Daudi wa Biblia alikuwa mtu halisi, na hivyo kufanya uvumbuzi huo wa kiakiolojia kuwa muhimu sana kati ya uvumbuzi wote wa nyakati za Biblia ulioripotiwa na BAR [Biblical Archaeology Review].”