Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

JW LUGHA

Maswali Yanayoulizwa Mara Nyingi​—JW Lugha (Android)

Maswali Yanayoulizwa Mara Nyingi​—JW Lugha (Android)

JW Lugha inaweza kutumiwa katika vifaa vifuatavyo:

  • Tablet na simu zenye mfumo wa Android (toleo la 5.0 au la karibuni zaidi)

  • Kindle Fire

Utegemezo kwa vifaa vifuatavyo hautapatikana:

  • Tablet na simu zenye mfumo wa Android toleo la 4.4 na la zamani zaidi

 

Unaweza kupakua habari katika JW Lugha ukitumia Wi-Fi au Intaneti ya simu. Katika menyu kuu, bofya Mipangilio. Kisha, chagua kitu unachotaka kwenye menyu karibu na sehemu Pakua.

 

Uwezo wa kuchagua mwendo wa sehemu ya kusikiliza unapatikana kwenye vifaa vinavyotumia Android 6.0 au vya kisasa zaidi. Chagua Mipangilio kwenye menyu kuu, kisha utumie menyu ndogo kando ya Mwendo wa Kucheza Rekodi (Global Playback Speed) kuchagua mwendo unaotaka. Unapofanya mazoezi, chagua mwendo kwenye zoezi hilo.

 

Hapana. Ili kupunguza sehemu inayotumiwa na kifaa chako kuhusiana na JW Lugha:

  • Pakua machapisho hususa tu badala ya kupakua machapisho yote

  • Pakua video zenye ubora mdogo

 

Rekodi ya kusikiliza katika sehemu ya Msamiati inatumia uwezo wa kifaa chako wa kubadili maandishi kuwa rekodi ya kusikiliza (TTS). Huenda ukahitaji kuweka programu tofauti ya TTS ili usikilize usomaji kwenye mfumo wenye ubora wa juu zaidi katika lugha unayojifunza. Mwendo wa kucheza unaweza kubadilishwa kwenye programu ya JW Lugha.

 

Mambo fulani kama vile kubadili mwendo wa kusikiliza, yanapatikana kwenye vifaa vya Android 6.0 au vya kisasa zaidi.

Ona pia: Je, programu hii itafanya kazi kwenye kifaa changu cha mkononi?

 

Lugha kuu ni lugha unayoijua. Unapoanza, chagua Lugha Kuu.

Tazama pia: Ninaweza kubadili lugha kuu jinsi gani?

 

Chagua Mipangilio kwenye menyu kuu, kisha ubadili lugha chini ya Lugha ya Kwanza.

 

Unapopakua Jw Lugha, utaombwa uchague lugha unayotaka kujifunza.

Tazama pia: Ninaweza kubadili lugha ya kwanza jinsi gani?

 

Chagua lugha katika sehemu ya kuchagua lugha.

Ona pia: Je, ninaweza kutumia lugha zaidi ya moja?

 

Ndiyo, unaweza kutumia lugha nyingi wakati uleule. Bofya sehemu ya kuchagua lugha na kisha uchague lugha ya ziada.

Ona pia: Ninaweza kubadili lugha jinsi gani?

 

Bofya menyu karibu na neno, fungu la maneno, au picha, kisha uchague Ongeza kwenye Mkusanyo. Bofya Tengeneza Mkusanyo Mpya ili upange habari jinsi unavyopenda na uipe jina. Unapoongeza mafungu ya maneno ukiwa kwenye Mtandao, habari hizo zinapakuliwa moja kwa moja kwenye kifaa chako ili uzipate bila Intaneti.

 

Bofya menyu kando ya kile unachotaka kunakili au kuondoa. Kisogeze ili upange upya mkusanyo.

 

Ndani ya mkusanyo, bofya Anza Mazoezi ili uone mazoezi yaliyomo:

  • Tazama: Chagua tafsiri ya neno unaloona

  • Patanisha: Chagua maneno yanayofanana na picha, au maneno na tafsiri ya maneno hayo

  • Sikiliza: Sikiliza fungu la maneno na uchague tafsiri sahihi

  • Kadi za Sauti: Fikiria tafsiri ya neno kabla ya kuangalia jibu. Badili mwendo wa kusikiliza unaposikiliza tena. Bofya sehemu ya sauti ili kuchagua kusikiliza tena.

  • Somo la Kusikiliza: Sikiliza maneno yakisomwa kwa sauti.

  • Bofya sehemu ya Hariri ili kusikiliza kwa mfuatano uliochaguliwa au kuchagua mfuatano unaotaka.

 

Ndiyo. Bofya Mipangilio kwenye menyu kuu, kisha utumie sehemu iliyoandikwa Onyesha Maandishi ya Kiroma (Show Romanization) ili kubadili maandishi ya Kiroma.

 

Maandishi yanapatikana muda wote, hata ikiwa hutumii Mtandao. Unapokuwa kwenye Mtandao, bofya fungu la maneno ili kuyasikiliza moja kwa moja. Ili kupakua video na habari za kusikiliza, bofya alama ya kupakua. Ili upakue video na habari zote za kusikiliza katika lugha unayojifunza, kuna maneno Pakua Yote sehemu ya kuchagua lugha, kando ya lugha unayotaka kujifunza.

 

Ndiyo, unaweza kuwa na nakala ya mkusanyo na historia. Katika menyu ya Mipangilio, chagua Hifadhi na Urudishe. Ikiwa tayari unanakili habari zako, unaweza kuzirudisha wakati wowote. Ukirudisha mkusanyo wenye jina sawa na mkusanyo mwingine kwenye kifaa chako, mkusanyo ulio kwenye kifaa utapotea.

 

Unaweza kumwomba rafiki anayejua jinsi ya kutumia programu ya JW Lugha akusaidie. Hilo likishindikana, tafadhali jaza na utume fomu yetu ya msaada mtandaoni