Mashahidi wa Yehova Ulimwenguni Pote

Korea, Jamhuri ya

  • Samcheong-dong, Seoul, Korea Kusini—Kufundisha kwa kutumia Biblia

  • Kijiji cha Daraengi, Kisiwa cha Namhae-do, Korea Kusini​—Kutoa broshua Msikilize Mungu

  • Nonsan-si, Chungnam, Korea Kusini​—Kushiriki ujumbe wa Biblia na mwenye nyumba anayekusanya chakula kutoka kwenye vyungu.

Taarifa Fupi—Korea, Jamhuri ya

  • 51,408,000—Idadi
  • 106,161—Wahudumu Wanaofundisha Biblia
  • 1,252—Makutaniko
  • 1 kwa 485—Uwiano wa Mashahidi wa Yehova kwa kulinganishwa na idadi ya watu nchini

TAARIFA ZA HABARI

Msimamo wa Kikristo wa Kutounga Mkono Upande Wowote Nchini Korea Kusini​—Historia ya Imani na Ujasiri

Tangu mwaka wa 1953, akina ndugu vijana nchini Korea ambao ni Mashahidi wa Yehova wamefungwa kwa kukataa utumishi wa kijeshi kwa sababu ya dhamiri. Mnamo Februari 2019, hali hiyo ilibadilika. Jifunze ni nini kilichoongoza kwenye tukio hilo la kihistoria.

TAARIFA ZA HABARI

Mashahidi wa Yehova Waadhimisha Miaka 100 Nchini Korea Kusini

SEOUL, Korea—Novemba 2012 ni mwezi wa pekee kwa Mashahidi wa Yehova zaidi ya 100,000 nchini Korea Kusini kwa kuwa wanaadhimisha mwaka wao wa 100 nchini humo.