Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Ustadi wa Kuogelea wa Samoni

Ustadi wa Kuogelea wa Samoni

Je, Ni Kazi ya Ubuni?

Ustadi wa Kuogelea wa Samoni

● Samoni wengi huogelea dhidi ya mkondo wa maji yenye msukosuko ili kwenda kutaga mayai. Ni nini kinachowawezesha kustahimili safari hiyo ngumu? Badala ya kulemewa na mkondo wenye nguvu wa maji, samaki hao hutumia mkondo huo kwa faida yao. Jinsi gani?

Fikiria hili: Samoni hawakati katikati ya maji hayo yenye msukosuko. Badala yake, wanapoogelea dhidi ya mkondo wa maji, wao huhifadhi nishati yao kwa kutumia mawimbi ya maji yanayozunguka kwa kasi mkondo wa maji unapokatizwa na miamba, matawi, au vitu vingine. Mawimbi hayo yanapotokea pande zote mbili za kizuizi, samoni hupinda-pinda mwili wake na kupitia katikati ya mawimbi hayo. (Ona picha.) Vikundi fulani vya samaki huogelea kwenye mawimbi yanayofanyizwa na samaki wanaoogelea mbele yao. Zaidi ya hilo, samaki wanaweza kuogelea kwenye mawimbi wanayotokeza wao wenyewe!

Watafiti wanatumaini kutumia ustadi wa kuogelea wa samoni ili kutokeza nishati kutoka kwa maji yanayoenda polepole. Kwa kawaida, mashini ya kutokeza umeme majini hutokeza umeme katika maji yanayosonga kwa mwendo wa kilomita 9.3 kwa saa, au kwa kasi zaidi. Sasa mashini inayofanyiza mawimbi ya maji inaweza kutokeza umeme katika maji yanayotiririka polepole kwa mwendo wa kilomita 3.7 kwa saa. * Hata hivyo, teknolojia hiyo haiwezi kufikia ustadi wa kuogelea wa samaki kama samoni. Profesa Michael Bernitsas wa Chuo Kikuu cha Michigan, Marekani anakiri hivi: “Hadi sasa, hatujafikia ustadi wa samoni.”

Una maoni gani? Je, uwezo wa samoni wa kuhifadhi nishati kwenye maji yenye msukosuko ulijitokeza wenyewe? Au ulibuniwa?

[Maelezo ya Chini]

^ fu. 5 Hayo ni matumaini mazuri kwa kuwa maji mengi duniani husafiri kwa mwendo wa kilomita 5.5 kwa saa.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 25]

Top: © photolibrary. All rights reserved.