Hamia kwenye habari

Ibilisi Ana Mwonekano Gani?

Ibilisi Ana Mwonekano Gani?

Jibu la Biblia

 Ibilisi ni kiumbe wa roho asiyeonekana, hilo linamaanisha hana mwili wa nyama ambao tunaweza kuuona.—Waefeso 6:11, 12.

 Wasanii wengi wamemchora Ibilisi kama kiumbe anayefanana na mbuzi mwenye pembe na mkia, na ameshika mti mrefu wenye meno. Baadhi ya watu wamesema kwamba michoro hiyo ilichorwa miaka 1000 hivi iliyopita na watu ambao huenda waliathiriwa na hadithi na hekaya za kale.

 Biblia inamfafanuaje Ibilisi?

 Biblia inatumia njia kadhaa kumfafanua Ibilisi. Mifano hiyo inatusaidia kuelewa utu wake, si mwonekano wake. Baadhi ya mifano hiyo ni:

  •   Malaika wa nuru. Anajaribu kufanya watu wafuate mafundisho yake badala ya mafundisho ya Mungu kwa kujifanya anawapa kitu bora.—2 Wakorintho 11:14.

  •   Simba anayenguruma. Anawashambulia vikali waabudu wa Mungu.—1 Petro 5:8.

  •   Joka mkubwa. Anatisha, ni mwenye nguvu, na husababisha uharibifu.—Ufunuo 12:9.