Hamia kwenye habari

Sera ya Ulimwenguni Pote ya Matumizi ya Vidakuzi na Teknolojia Sawa

Sera ya Ulimwenguni Pote ya Matumizi ya Vidakuzi na Teknolojia Sawa

Ili ufurahie kutumia tovuti hii, huenda tukahifadhi au kupata kiasi kidogo cha taarifa kutoka kwenye katika simu yako, tablet, au kwenye kompyuta yako kwa kutumia vidakuzi na teknolojia zinazofanana na hizo. Vidakuzi vinaiwezesha tovuti hii ifanye kazi na kutupatia taarifa kuhusu jinsi mtumiaji anavyotumia tovuti yetu. Tunatumia taarifa hizo kuboresha tovuti yetu. Hatutafuti habari hizo ili kupata taarifa za kibinafsi za mtu anayetembelea tovuti yetu isipokuwa iwe mtu huyo alitoa taarifa zake kwa hiari kwa kujaza mojawapo ya fomu au maombi yaliyoko kwenye tovuti. Matumizi ya neno “vidakuzi” (cookies) katika Sera hii ni mapana na yanatia ndani teknolojia sawa kama ile ya localStorage, web beacons, pixels, na identifiers. Hizi teknolojia sawa zinaweza kutupa taarifa kuhusu habari zilizo kwenye kompyuta yako kama vile, ukubwa wa skrini ya kompyuta yako, tarehe na muda ulioingia kwenye tovuti, na URL ya kurasa uliyofungua.

Taarifa tutakazohifadhi au kupata kutoka kwenye kifaa chako hazitauzwa kamwe, wala kutumiwa kibiashara, au kutumiwa ili kuhifadhi habari kuhusu tovuti nyingine ulizotembelea mtandaoni. Hatutumii vidakuzi vya matangazo yaliyokusudiwa mtu mlengwa au vidakuzi vya kibiashara.

Aina za Vidakuzi. Kuna aina mbalimbali za vidakuzi vinavyofanya kazi mbalimbali na kwa ujumla vinaboresha jinsi unavyotumia tovuti. Tunatumia vidakuzi kujua ikiwa uliwahi kutembelea tovuti yetu au kuweka kumbukumbu ya mapendezi unayochagua unapotumia tovuti yetu. Kwa mfano, tunaweza kuhifadhi lugha unayochagua kutumia katika kidakuzi ili uitumie unapotembelea tena tovuti yetu.

Vidakuzi vinavyotumiwa katika tovuti hii vinaweza kugawanywa katika makundi matatu:

  1. Vidakuzi Muhimu Sana. Baadhi ya vidakuzi ni muhimu ili kuwezesha tovuti yetu kufanya kazi, pia vinamwezesha mtu kurambaza mambo mbalimbali kwenye tovuti yetu, au kutumia sehemu mbalimbali katika tovuti. Kwa kawaida vinatumika unapoomba huduma fulani kama vile kubadilisha mipangilio inayohusu faragha yako, kuingia kwenye akaunti, au kujaza fomu. Bila vidakuzi hivi, usingeweza kupata baadhi ya huduma ambazo ungependa kutumia, kama vile kutoa mchango kwa njia ya mtandao. Vidakuzi hivi havihifadhi taarifa zako za kibinafsi ambazo zinaweza kutumiwa kibiashara au kujulisha wengine tovuti ulizotembelea.

  2. Vidakuzi vya Utendaji. Hivi husaidia tovuti kukumbuka mambo unayoingiza (kwa mfano jina, lugha, au mahali) na hivyo, utafurahia zaidi kutumia sehemu mbalimbali katika tovuti hii. Vidakuzi hivi vinakurahisishia mambo mengi kwenye tovuti yetu, vinakusaidia unaporambaza, na kukuruhusu kuchagua mapendezi yatakayokusaidia kutumia tovuti yetu kwa njia itakayokufurahisha.

  3. Vidakuzi vya Uchanganuzi na Vinavyohifadhi Takwimu ya Utumiaji. Hivi vinatumika kukusanya takwimu za jinsi wale wanaotembelea tovuti wanavyoitumia. Takwimu hizo zinatia ndani taarifa kama vile ni mara ngapi tovuti imetembelewa au mtu aliyeitembelea aliitumia kwa muda gani. Taarifa hizo hukusanywa tu ili kuboresha utendaji wa tovuti, kutia ndani muundo wa tovuti, uwezo wa tovuti kufungua kurasa haraka, na miundombinu mingine.

Vidakuzi vingi tunavyotumia ni vya mtu wa kwanza, navyo vinawekwa na tovuti yetu. Vingine ni vidakuzi vya mtu wa tatu, navyo huwekwa na tovuti nyingine. Katika orodha yetu ya mifano ya vidakuzi, tunatambulisha waziwazi vidakuzi vya mtu wa tatu.

Matumizi ya Anwani ya IP. Anwani ya IP ni mfululizo wa namba kadhaa zinazotambulisha kifaa chako unapokuwa mtandaoni. Tunatumia anwani yako ya IP, na pia, aina ya kivinjari chako kutusaidia kuchunguza matumizi ya tovuti, kugundua matatizo yanayotokea katika tovuti, kuboresha huduma tunayokupatia, na kulinda usalama wa tovuti.

Uchaguzi Wako. Unaweza kubadili vidakuzi vilivyopo wakati wowote kwa kufungua “Mipangilio ya Faragha” (Privacy Settings) iliyo mwishoni mwa ukurasa huu. Ni vidakuzi muhimu tu ambavyo huwezi kubadili. Lakini inapohusu aina nyingine ya vidakuzi, tunaomba ruhusa yako kabla ya kuviruhusu kuhifadhi taarifa au kupata taarifa kutoka kwa kifaa chako. Tafadhali zingatia kwamba kubadili mipangilio hiyo ya faragha, hakufuti vidakuzi vilivyopo. Ikiwa utapenda kufuta vidakuzi kwenye tovuti hii, unaweza kufanya hivyo kupitia sehemu ya mipangilio katika kivinjari chako. Hata hivyo, tafadhali zingatia kwamba bila kuwa na vidakuzi hutaweza kutumia vizuri baadhi ya sehemu zinazopatikana katika tovuti yetu. Njia za kufuta kidakuzi zinatofautiana kati ya kivinjari kimoja na kingine. Unaweza kuangalia sehemu ya Msaada katika kivinjari chako ili upate miongozo kamili au unaweza kutembelea www.allaboutcookies.org.

Chagua mojawapo ya tovuti zilizopo kwenye orodha iliyo hapa chini ili uone mifano ya matumizi ya vidakuzi katika tovuti.

Ona pia Vidakuzi na Teknolojia Sawa Zinazotumiwa na Tovuti Zetu Mbalimbali.