Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

JW LIBRARY

Pakua na Utumie Machapisho​—Windows

Pakua na Utumie Machapisho​—Windows

Kuna mamia ya vitabu, broshua, trakti unazoweza kusoma na video unazoweza kutazama kwenye JW Library hata wakati ambapo umezima intaneti.

Fuata maelekezo yafuatayo ili kupakua na kutumia machapisho:

 Pakua Machapisho

Unaweza kupakua machapisho mengi kadiri unavyotaka ili usome na kujifunza unapozima intaneti.

  • Kwenye sehemu ya juu ya skrini yako, bofya Machapisho na kisha bofya Aina ili kupata orodha ya machapisho.

  • Fungua Amri za Programu, kisha bofya kitufe cha Lugha ili kuona orodha ya lugha mbalimbali ambazo unaweza kupata machapisho katika lugha hizo. Chagua lugha unayotaka kuona. Lugha unazotumia mara nyingi sana zinakuwa mwanzoni mwa orodha. Pia unaweza kutafuta lugha unayotaka kwa kuandika jina la lugha unayotafuta.

Kuna njia kadhaa za kutafuta machapisho kwenye JW Library.

Sehemu ya Aina inaonyesha machapisho ya lugha uliyochagua, yakiwa yamewekwa kulingana na aina kama vile Vitabu, Trakti, au Video. Ukibofya aina fulani utapata uchaguzi wa ziada, kwa mfano ukibofya Mnara wa Mlinzi utapata mpangilio kulingana na mwaka au sehemu ya video itakupa aina mbalimbali za Video. Bofya Aina Zote ili kurudi kwenye orodha ya machapisho yote.

Sehemu ya Nini Kipya inaonyesha machapisho ambayo yametolewa hivi karibuni katika lugha uliyochagua.

Machapisho ambayo bado hayajapakuliwa yana alama ya wingu. Bofya chapisho ikiwa unataka kulipakua. Mara baada ya chapisho kupakuliwa katika kifaa chako, alama ya wingu inatoweka. Bofya tena chapisho hilo ili ulisome.

Sehemu ya Yaliyopakuliwa inaonyesha machapisho yote uliyopakua katika lugha yoyote. Unaweza kutenganisha sehemu hii kwa Yanayotumika kwa Ukawaida, Ambayo Hutumii kwa Ukawaida, au Makubwa.

 Futa Chapisho

Unaweza kufuta chapisho ikiwa hulihitaji tena, au ikiwa unataka kupata nafasi zaidi.

Kwenye sehemu ya juu ya skrini, bofya Machapisho, kisha bofya Aina ili kuona orodha ya machapisho. Gusa na ubofye chapisho hilo ili kulichagua. Bofya Futa kwenye Amri za Programu, kisha thibitisha kwamba unataka kufuta chapisho hilo.

Ikiwa unataka kupata nafasi zaidi kwenye kifaa chako, unaweza kufuta machapisho usiyotumia kwa ukawaida au machapisho makubwa sana. Bofya Machapisho, kisha bofya Yaliyopakuliwa, kisha panga orodha kulingana na Ambayo Hutumii kwa Ukawaida au Makubwa. Futa machapisho ambayo huhitaji.

 Sasisha Chapisho

Mara kwa mara, chapisho ambalo umepakua hurekebishwa au matoleo mapya huingizwa.

Chapisho ambalo limerekebishwa huwa na alama ya vishale. Unapobofya chapisho hilo, utaona ujumbe unaosema kwamba chapisho hilo limerekebishwa. Bonyeza Pakua ili kusasisha au, bonyeza Baadaye ili kuendelea kusoma toleo ambalo ulipakua.

Ili kuona ikiwa chapisho lolote ulilopakua limerekebishwa, bofya Machapisho. Ikiwa kuna machapisho yaliyorekebishwa, sehemu yenye kichwa Sasisha itakuwepo. Bofya uone orodha yote ya machapisho yanayohitaji kusasishwa. Bofya chapisho moja ili kulisasisha, au ubofye kitufe cha Sasisha Yote ili upakue machapisho yote yaliyorekebishwa.

Sehemu hizo mbalimbali zilipatikana Machi 2015 kwenye JW Library toleo la 1.4, ambalo linafanya kazi vizuri kwenye vifaa vinavyotumia mfumo wa Windows 8.1 au wa karibuni zaidi. Ikiwa hauoni mambo haya, tafadhali fuata mwelekezo kwenye makala “Anza Kutumia JW Library​—Windows,” kwenye Pata Habari za Karibuni Zaidi.