Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

John Moore/Getty Images

KAMPENI YA PEKEE

Ufalme wa Mungu Utafanya Nini Kuhusu Matatizo ya Afya?

Ufalme wa Mungu Utafanya Nini Kuhusu Matatizo ya Afya?

 “Ingawa makali ya COVID-19 yamepungua ulimwenguni kote, hilo halimaanishi kwamba COVID-19 imeacha kuwa tishio.. . . Ukweli ni kwamba, janga lingine litakuja na tunahitaji kuwa tayari.”​—Dakt. Tedros Adhanom Ghebreyesus, mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Ulimwenguni, Mei 22, 2023.

 Watu wengi bado wanaendelea kupambana na athari za kimwili na kiakili walizopata kutokana na janga la COVID-19. Je, kweli serikali na taasisi za afya zitaweza kukabiliana na janga lingine huku zikishughulikia matatizo ya afya ambayo tayari tunayo?

 Biblia inatueleza kwamba kuna serikali ambayo itatatua matatizo ya afya. Inasema kwamba “Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme,” yaani, serikali. (Danieli 2:44) Chini ya Ufalme huo, “hakuna mkaaji atakayesema: “Mimi ni mgonjwa.” (Isaya 33:24) Kila mtu atakuwa na afya nzuri na nguvu za ujana.​— Ayubu 33:25.