APRILI 23, 2024
URUSI
Tunathamini Sana Pendeleo la Kumtumikia Yehova
Mahakama ya Pervomayskiy iliyo katika Wilaya ya Izhevsk katika Jamhuri ya Udmurtian, itatangaza uamuzi wake katika kesi inayowahusu Ndugu Yevgeniy Stefanidin na Ndugu Aleksandr Votyakov. Mwendesha mashtaka bado hajatoa ombi la hukumu anayopendekeza.
Maelezo Mafupi Kuwahusu
Kama Aleksandr na Yevgeniy, tunaliona kuwa pendeleo kubwa “Kumtolea [Yehova] utumishi mtakatifu bila woga” siku zetu zote.—Luka 1:74, 75.
Mfuatano wa Matukio
Aprili 14, 2021
Maofisa wa usalama walifanya msako kwenye nyumba ya Yevgeniy
Desemba 13, 2022
Kesi ya uhalifu ilifunguliwa dhidi ya Aleksandr na Yevgeniy
Desemba 14, 2022
Maofisa walifanya msako kwenye nyumba ya Aleksandr na ya Yevgeniy. Aleksandr alipelekwa mahabusu. Yevgeniy aliwekewa vizuizi vya kusafiri
Desemba 15, 2022
Aleksandr aliachiliwa kutoka mahabusu na akawekwa katika kifungo cha nyumbani
Juni 9, 2023
Aleksandr aliachiliwa kutoka katika kifungo cha nyumbani na akawekewa vizuizi vya kusafiri
Agosti 17, 2023
Kesi ya uhalifu ilianza