Hamia kwenye habari

Ndugu Yevgeniy Bushev

NOVEMBA 20, 2023
URUSI

Ndugu Yevgeniy Bushev Alihukumiwa Kifungo cha Miaka Saba Gerezani

Ndugu Yevgeniy Bushev Alihukumiwa Kifungo cha Miaka Saba Gerezani

Novemba 7, 2023, Mahakama ya Wilaya ya Kalininskiy iliyo katika Eneo la Chelyabinsk ilimhukumu Ndugu Yevgeniy Bushev kifungo cha miaka saba gerezani. Alipelekwa gerezani moja kwa moja kutoka mahakamani.

Maelezo Mafupi Kumhusu

Tunasikitika kwamba ndugu yetu mwingine anapelekwa gerezani. Hata hivyo, hatuna shaka kwamba Yehova ataendelea kuwa kimbilio na mwamba wa Yevgeniy.​—Zaburi 94:22.

Mfuatano wa Matukio

  1. Agosti 24, 2022

    Kesi ya uhalifu ilifunguliwa

  2. Septemba 8, 2022

    Nyumba ilifanyiwa upekuzi

  3. Septemba 9, 2022

    Aliwekewa vizuizi vya kusafiri

  4. Septemba 20, 2023

    Kesi ya uhalifu ilianza

  5. Novemba 7, 2023

    Alihukumiwa kifungo cha miaka saba gerezani