Hamia kwenye habari

Ndugu Kirill Gushchin na mke wake, Svetlana

MACHI 9, 2022
URUSI

Kusali kwa Ajili ya Wakristo Wenzake Kunamwimarisha Ndugu Kirill Gushchin

Kusali kwa Ajili ya Wakristo Wenzake Kunamwimarisha Ndugu Kirill Gushchin

Mahakama ya Jiji la Mayskiy ya Jamhuri ya Kabardino-Balkaria hivi karibuni itatangaza uamuzi wake katika kesi inayomhusu Ndugu Kirill Gushchin.

Mfuatano wa Matukio

  1. Mei 20, 2020

    Kirill alipokuwa akielekea kazini, maofisa wa FSB waliojifunika uso na wenye silaha walimzunguka. Maofisa hao walimfunga pingu na wakamrejesha nyumbani kwake. Kirill na mke wake, Svetlana, walifungiwa kwenye chumba kimoja huku nyumba yao ikipekuliwa. Ofisa mmoja alificha machapisho yaliyopigwa marufuku ndani ya chumba chao cha kulala na chumba kingine pia

  2. Aprili 26, 2021

    Wenye mamlaka walifungua kesi ya uhalifu dhidi ya Kirill wakitegemea ushahidi uliotolewa na mtu fulani aliyekuwa amerekodi mikutano kisiri. Mpelelezi alimshtaki Kirill kwa kuimba na kusali na pia kuzungumzia ushauri mzuri wa Biblia unaopatikana katika 1 Wakorintho 13:8: “Upendo haushindwi kamwe.”

  3. Aprili 28, 2021

    Wenye mamlaka walimshtaki Kirill kirasmi kwa shtaka la uhalifu. Kesi nyingine ya uhalifu ilifunguliwa dhidi ya Svetlana na dada wengine wanne

  4. Mei 19, 2021

    Mmoja wa maofisa wa FSB ambaye alihusika katika uchunguzi wa kesi hiyo, alishtakiwa kwa kutisha mashahidi. Hapo awali alipatikana na hatia ya kutoa ushahidi wa uwongo dhidi ya Mashahidi wa Yehova. Mkuu wa Idara ya Upelelezi aliamuru kwamba kesi hiyo irudishwe kwa mwendesha-mashtaka ili ifanyiwe uchunguzi zaidi

  5. Juni 7, 2021

    Kwa mara nyingine, kesi hiyo ililetwa tena kwenye Mahakama ya Wilaya ya Mayskiy

Maelezo Mafupi Kumhusu

Kama Kirill, tuna uhakika kwamba Yehova atakuwa “kimbilio salama katika nyakati za taabu” kwake yeye, na pia kwa ndugu na dada zetu wote wanaovumilia mateso nchini Urusi na Crimea.​—Zaburi 9:9, 10.