Hamia kwenye habari

Ndugu Aleksandr Dolganov

APRILI 4, 2024 | HABARI ZIMEONGEZWA: APRILI 9, 2024
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU AHUKUMIWA | ‘Jambo Muhimu Ni Kudumisha Urafiki Wangu na Yehova’

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU AHUKUMIWA | ‘Jambo Muhimu Ni Kudumisha Urafiki Wangu na Yehova’

Aprili 8, 2024, Mahakama ya Wilaya ya Avtozavodskiy katika mji wa Tolyatti iliyo katika Eneo la Samara ilimhukumu Ndugu Aleksandr Dolganov kifungo cha miaka mitatu gerezani. Alipelekwa gerezani moja kwa moja kutoka mahakamani.

Maelezo Mafupi Kumhusu

Kama Aleksandr, sisi pia tunaona ni muhimu kutumia vizuri wakati wetu katika ‘siku hizi zenye uovu.’​—Waefeso 5:15, 16.

Mfuatano wa Matukio

  1. Mei 16, 2023

    Nyumba ilifanyiwa msako. Aleksandr alipelekwa kuzuizini

  2. Mei 17, 2023

    Aliachiliwa kutoka kizuizini na kuwekwa katika kifungo cha nyumbani. Hakuruhusiwa kutumia simu au intaneti

  3. Agosti 10, 2023

    Aliachiliwa kutoka katika kifungo cha nyumbani na akawekewa vizuizi vya kusafiri

  4. Novemba 13, 2023

    Kesi ya uhalifu ilianza