Hamia kwenye habari

MACHI 5, 2020
HABARI ZA ULIMWENGUNI POTE

Ripoti ya Halmashauri ya Waratibu ya 2019​—Kutegemeza Ndugu Zetu Majanga Yanapotokea

Ripoti ya Halmashauri ya Waratibu ya 2019​—Kutegemeza Ndugu Zetu Majanga Yanapotokea

Ripoti ya Halmashauri ya Waratibu ya 2019 yenye kichwa Kutegemeza Ndugu Zetu Majanga Yanapotokea inaonyesha jinsi tengenezo letu linavyosaidia undugu wa ulimwenguni pote kushughulikia dharura. Ripoti hii inatia ndani habari kuhusu jinsi ndugu zetu walivyojitolea kusaidia baada ya tetemeko la ardhi na tsunami zilizotokea nchini Indonesia na mlipuko wa homa ya manjano nchini Nigeria. Na hata wakati huu ugonjwa unaoenea kwa kasi wa virusi vya corona (inayoitwa pia COVID-19), Baraza Linaloongoza litaendelea kutoa mwongozo kwa ajili na ndugu na dada wanaoishi katika maeneo yaliyoathiriwa na ugonjwa huo duniani pote.