Hamia kwenye habari

MEI 8, 2024
HABARI ZA ULIMWENGUNI POTE

Mvua Kubwa Zasababisha Mafuriko Makubwa Nchini Kenya na Tanzania

Mvua Kubwa Zasababisha Mafuriko Makubwa Nchini Kenya na Tanzania

Katika mwezi wa Aprili, 2024, mvua kubwa imenyesha nchini Kenya na Tanzania na kusababisha mafuriko makubwa. Zaidi ya watu 185,000 wamelazimika kuhama makao yao nchini Kenya na watu 200 hivi wamepoteza uhai wao. Pia, inakadiriwa kwamba katika nchi jirani ya Tanzania, watu 200,000 wamelazimika kuhama makao yao na watu 200 hivi wamekufa. Inatarajiwa mvua kubwa zaidi itaendelea kunyesha katika majuma yajayo.

Athari Ambazo Ndugu na Dada Zetu Wamepata

  • Kwa kusikitisha, dada 1 na binti yake walikufa

  • Wahubiri 59 wamelazimika kuhama makao yao

  • Nyumba 14 zimepata uharibifu mkubwa

  • Majumba 3 ya Ufalme na jengo 1 la shule ya kitheokrasi limeharibiwa

Jitihada za Kutoa Msaada

  • Waangalizi wa mzunguko wanashirikiana na wazee kutoa msaada wa kiroho na wa kimwili kwa wale walioathiriwa na mafuriko hayo

Tunaendelea kusali kwa ajili ya ndugu na dada walioathiriwa na msiba huu wa asili. Ingawa tunaishi katika nyakati ngumu, tuna uhakika kwamba hivi karibuni ‘hatutaogopa chochote na hatutakuwa na sababu yoyote ya kuhofu.’​—Isaya 54:14.