Hamia kwenye habari

Kushoto kwenda kulia: Ndugu Yuriy Kolotinskiy, Ndugu Mikhail Reshetnikov, na Ndugu Anatoliy Sarychev

MACHI 27, 2024 | HABARI ZIMEONGEZWA: MEI 13, 2024
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU WAHUKUMIWA | Walikuwa na Uhakika, Walijitayarisha, na Walikuwa na Mtazamo Mzuri

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU WAHUKUMIWA | Walikuwa na Uhakika, Walijitayarisha, na Walikuwa na Mtazamo Mzuri

Mei 13, 2024, Mahakama ya Leninskiy ya Wilaya ya Barnaul iliyo katika Eneo la Altai iliwahukumu Ndugu Yuriy Kolotinskiy, Ndugu Mikhail Reshetnikov, na Ndugu Anatoliy Sarychev. Kila mmoja alipokea kifungo cha nje cha miaka miwili na miezi mitatu. Hawahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Tunafurahi sana kuwa na ndugu kama hawa, ambao ni mifano mizuri ya imani na kumtegemea Yehova katika siku zetu. Tuna uhakika kwamba wataendelea kunufaika na upendo mshikamanifu wa Yehova na uaminifu.​—Zaburi 25:10.

Mfuatano wa Matukio

  1. Mei 25, 2021

    Kesi ya uhalifu ilifunguliwa dhidi ya Mikhail

  2. Mei 27, 2021

    Nyumba ya Mikhail ilifanyiwa msako. Yeye na Antonina walihojiwa. Mikhail aliwekewa vizuizi vya kusafiri

  3. Oktoba 6, 2022

    Kesi ya uhalifu ilifunguliwa dhidi ya Anatoliy na Yuriy na ikaunganishwa pamoja na kesi ya Mikhail

  4. Oktoba 7, 2022

    Anatoliy na Yuriy waliwekewa vizuizi vya kusafiri

  5. Januari 19, 2023

    Kesi ya uhalifu ilianza